Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama
barabarani Tanzania, mohammed Ramadhan Mpinga, akitoa elimu ya usalama bararani
kwa waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya
kombe la Mpinga Cup 2016 kutoka kundi E, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata
Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).
Msaidizi wa Kamanda DCP Mpinga, SACP
Fortunatus Muslim, akitoa elimu ya
usalama bararani kwa waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa
mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 kutoka kundi E, iliyofanyika kwenye
uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).
S/SGT Enock Machunde, Kitengo cha
Elimu kutoka Traffic Makao Makuu Dar es Salaam,
akitoa elimu ya usalama bararani kwa wachezaji wa timu zilizoshiriki
kundi E ambao ni waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa
mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata
Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).
PC Abdallah Ismail, Kitengo cha Elimu
kutoka Traffic Makao Makuu, akitoa elimu
ya usalama bararani kwa wachezaji kabla ya kuingia Uwanjani wakati wa
mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 yanayoshirikisha waendesha pikipiki
maarufu kama bodaboda, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha
na Traffic Makao Makuu).
Mwenyekiti wa chama cha waendesha
pikipiki kutoka mkoa wa Kipolisi Ilala, Mademla Bang’ala, akifafanua jambo
kabla ya michezo hiyo kwenye michezo ya kundi (E) timu za waendesha pikipiki
maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016
iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao
Makuu).
====================================
KAMANDA WA POLISI KIKOSI CHA USALAMA
BARABARANI (MOHAMED MPINGA) ATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA WA
BODABODA.
Na: Mwandishi Wetu.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama
barabarani Tanzania, Mohammed Ramadhani Mpinga, Juzi alikuwa ni miongoni mwa
Wakufunzi wa kutoa elimu ya Masuala ya Usalama Barabarani wakati wa mashindano
ya Mpinga Cup 2016 yanayohusisha madereva wa Pikipiki na bajaji kwa mkoa wa
Kipolisi wa Ilala jijini Dar es Salaam katika mfululizo wa michezo hiyo
inayoendelea katika viwanja mbalimbali.
Katika mashindano hayo jumla ya timu
59 tayari zimefanikiwa kusonga mbele hatua ya pili ya mtoano wa mashindano haya
ambayo mwishoni mwa wiki timu zilizocheza zilikuwa ni pamoja na Matunda fc
dhidi ya Zahanati ambapo mashindi alikuwa ni zahanati ,alipatikana kwa njia ya
penalt 5-4, wafungaji kwa upande wa
Zahanati wakiwa ni Fredy Chambogo, Isaac
Elisha, Musa Masho, Shiiko Rashifod , na mfungaji wa timu ya Matunda
walikuwa ni Shaaban Awami, Kelvin
Sweetbati, Salum MWaikimba, Yusuph Mohamed.
mchezo wa pili ulikuwa ni Kwa bibi fc
aliyecheza na Chama fc na Mshindi alikuwa ni Chama Fc kwa jumla ya 1-0, mfungaji
akiwa Amani kadodo dakika ya 18 kipindi cha kwanza, mchezo wa tatu
ulizikutanisha timu za Tabata Bodaboda na Tabata Old Trafford na mshindi
alikuwa ni timu ya Tabata Bodaboda kwa jumla ya mabao 3-1 wafungaji kwa upande
wa Traffod walikuwa Abdallah Hussen dk 27 kipindi cha kwanza, Miraji Sarehe dk
36 kipindi cha kwanza na goli la tatu
liliwekwa kimiani na Saidi Ngwira katika dakika za majeruhi.
Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya
Barakuda Kilimanjaro na Barakuda Fc ambapo mshindi alikuwa ni timu ya Barakuda
Kilimanjaro kwa ushindi wa mezani baada ya wapinzani kushindwa kutokea
uwanjani. Na mchezo uliofuata ulikuwa ni kati ya timu ya Liwiti fc dhidi ya
Luwi Safari fc ambapo mchindi alikuwa ni timu ya Liwiti fc waliopata ushindi wa
chee baada ya wapinzani kushindwa kutokea uwanjani.
Timu zilizofuatia katika ku hiyo ya
jumamosi ilikuwa ni kati ya Kinyerezi Saloon waliocheza na Mbuyuni Fc ambapo
matokeo katika mchezo huo timu ya mbuyuni waliibuka kidedea kwa ushindi wa
bao 1-0 mfungaji akiwa Kitenge Kitenge
aliyefunga dakika ya 16 kipindi cha kwanza na mchezo uliofuata ulizikutanisha
timu za Segerea SBG dhidi ya timu ya Segerea Sheli Bodaboda na matokeo katika
mchezo huo timu ya Segerea Sheli Bodaboda waliibuka mshindi wa 1-0 mfungaji
akiwa Jackson Hamadi dakika 25 kipindi cha pili.
Mashindano hayo yaliendelea tena siku
ya jumapili ambapo jumla ya timu kumi na mbili zilishiriki kuwania nafasi ya
kusonga mbele na mchezo wa kwanza ulikuwa ni kati ya Transpoter Fc iliyocheza
na Kecha Fc na Timu ya Kecha ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mfungaji
katika mchezo huo akiwa ni Mashaka Hamisi aliyefunga kwa shuti kali dakika 18
ya kipindi cha ili, huku ukifuatiwa na mchezo kati ya White Egle fc dhidi ya
timu ya Migombani Fc ambapo mchezo huo timu ya White Egle iliibuka na ushindi
wa mabao 8-7 baada ya kupigiana penalt kutokana na timu hizo kushindwa
kutambiana kwenye dakika 90 za mchezo baada ya kumaliza zikiwa zimefungana bao
1-1. Wafungaji kwa timu ya White Egle walikuwa ni Selemani Uswege, Elick Fod, Muso Uswege, Zuberi Hassani, Jofu Tito, Erick Sabuni, wafungaji
kwa upanda timu ya Migombani walikuwa ni Shaaban Hamisi, Juma Abdalah, Erick
Ndidi, Sifaeli Haule, Patrick Esau, Hamadi Msuyale na Dua Juma.
Akizungumzia mashindano hayo Mratibu
wa mashindano ASP Mbuja Saidi Matibu alisema kuwa, mpaka sasa mashindano hayo
yanaendelea vizuri na amewapongeza viongozi wa tmu kwa kuweza kufika kwa wakati
kwenye michezo yao na kwamba timu zote zimeshiriki na kukubali matokeo kwa timu
zote zilizofungwa, na pia wachezaji wamekuwa na hamasa ya hali ya juu na kuomba
mashindano haya kuwa endelevu, ili kuwafikia bodaboda kwa wingi ikiwezekana iwe
kwa nchi nzima.
Nae Mwenyekiti wa bodaboda mkoa wa
Kipolisi Ilala, Mademla Bang’ala alisema kuwa, wanamshukuru kamanda wa Polisi
kikosi cha usalama barabarani kwa niaba ya Jeshi la Polisi kwa kuwapa
changamoto madereva wa bodaboda kwa kujenga afya zao kwa njia hiyo ya michezo
na kuwapa elimu ya Usalama barabarani ili kuepukana na ajali za mara kwa mara,
na kwamba wanaomba mashindano haya yasiishie tu mkoa wa Dar es salaam na badala
yake yapelekwe kwenye Mikoa yote ya Tanzania.
Mchezo mwingine ulikuwa ni Buguruni
sheli fc Bodaboda waliocheza na timu ya Buguruni Sheli Bajaji mshindi katika
mchezo huo alikuwa ni timu Buguruni Sheli bajaji kwa jumla ya mabao 3-1,wafungaji
kwa upande wa timu ya bodaboda ni Willy Pashau na kwa upande wa Bajaji
wafungaji ni Abdul Ismail, moshi Shilingi, na Chrispofe Chibondo, mchezo
mwingine uliofuata siku ya jumapili ulikuwa ni kati ya timu Segerea Mangala Fc
waliocheza na timu ya Sanene fc na mshindi alikuwa ni timu ya Segerea Mangala
fc kwa njia ya matuta 3-1 wafungaji kwa uande wa Segerea mangala ni Abeid Musa,
Amani Saidi, Mbonde Ashilafu, baada ya kumaliza dakika 90 timu hizo zikiwa
zimefungana bao 1-1, hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa mabao 4-2 na wafungaji
kwa upande wa timu ya Sanene fc walikuwa ni Samba John na Mrisho Issa.
Wakati huo huo Afisa habari Msaidizi
wa timu za bodaboda Tito Razalo Mpiziwa amemshukuru kamanda wa Polisi Kikosi
cha Usalama barabarani kwa kuweza kufanikisha mashindano haya, ambayo kwa
muonekano tayari ni zaidi ya bodaboda 6000 wa mkoa wa Dar es salaam walioweza
kunufaika na mashindano haya kutokana na kupata mafunzo ya elimu ya usalama
barabarani.
Mchezo mwingine ulizikutanisha timu
za Kwetu pazuri fc na Segerea Kona Fc ambapo mshindi alikuwa ni timu ya Kwetu
Pazuri waliopata ushindi wa mezani baada ya wapinzani wao kushindwa kutokea
uwanjani , na mchezo uliofuata ulikuwa ni kati ya Pelalela fc waliocheza na
timu ya Relini kwa Mnyamani na mshindi alikuwa ni Timu ya Relini kwa Mnyamani
waliopata ushidi wa bure.
Mashindano haya yanadhaminiwa na
Baraza la Usalama Barabarani(T), Jeshi la Polisi Tanzania, Cool Blue Tanzania,
NMB, Zantel, Reb Bull, Windhoeck, Coc cola, Haki Elimu, Star Times, EFM Radio,
Michuzi Blogs, NHIF, BIG BON, GSM, T-Marc Tanzania, Bavaria, Chai Bora, Dar
City Promotions, Yono, Mwananchi Communications, Quality Group, Puma, TBL,
Milcom, My Way Entertainments, Balozi wa Demokrasia Tanzania, Miss Demokrasia
Tanzania, na MpaluleBlogs.

No comments:
Post a Comment